Msiingie miji ya wale waliozidhulumu nafsi zao, isipokuwa muwe mnalia
Islam > Sw > Hadith > Adabu za kisheria > Msiingie miji ya wale waliozidhulumu nafsi zao, isipokuwa muwe mnalia
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Msiingie miji ya wale waliozidhulumu nafsi zao, isipoku…
Maelezo ya hadith: Msiingie miji ya wale waliozidhulumu nafsi zao, isipoku…
Alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipopita katika miji ya Thamudi, kutoingia katika miji ya walioadhibiwa, wale waliozidhulumu nafsi zao au kuiendea miji hiyo, isipokuwa anayeingia kama atakuwa analia kwa kuchukua mazingatio kwao; kwa kuhofia asijekufikwa na mfano wa yale yaliyowafika miongoni mwa adhabu, kisha akampigia kelele mnyama wake akaongeza mbio mpaka akaivuka.
Mafunzo: Msiingie miji ya wale waliozidhulumu nafsi zao, isipoku…
- Kutafakari katika hali za wale aliowaangamiza Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuchukua tahadhari katika yale waliyotumbukia kwayo; na kuchukua tahadhari ya kujisahau kutozingatia alama.
- Miji ya hao walioadhibiwa haitakiwi kuishi baada yao, na wala haifanwyi kuwa makazi, kwa sababu atakayeishi hapo hawezi kulia daima, na ilikatazwa kuingia ila kwa sifa hii.
- Amesema Nawawi: Hapa kuna himizo la kuchunga wakati wa kupita katika miji ya madhalimu, na sehemu za adhabu, na mfano wake vile vile ni kwenda haraka katika bonde la Muhassiri (Liko Makkah, katika Mina na Muzdalifa); kwa sababu watu wa ndovu waliangamia huko, inatakiwa kwa mwenye kupita katika mfano wa sehemu hizi kuchunga na kuwa na hofu na kulia, na kuchukua mazingatio kwao na maangamizo yao, na aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na hilo.
- Katazo na tahadhari yanakusanya nyumba za Thamudi na wengineo wenye kufanana nao katika umma nyinginezo walioteremkiwa na adhabu.
- Katazo la kuzifanya sehemu na maeneo haya kuwa sehemu za utalii na matembezi na mfano wake.
Makundi :
Adabu za kisheria.
· Adabu na Hukumu za Safari.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
اللهم صل على محمد
Ô Allah prie sur Muhammad