Basi kusanyikeni katika chakula chenu, na mkitajie jina la Mwenyezi Mungu, mtabarikiwa kat…
Islam > Sw > Hadith > Adabu za kisheria > Basi kusanyikeni katika chakula chenu, na mkitajie jina la Mwenyezi Mungu, mtabarikiwa kat…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad
Ni nzuri (Hasan)
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Basi kusanyikeni katika chakula chenu, na mkitajie jina…
Maelezo ya hadith: Basi kusanyikeni katika chakula chenu, na mkitajie jina…
Baadhi ya Maswahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakasema: Hakika sisi tunakula lakini hatushibi.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kuwaambia: Huenda nyinyi kila mtu hukaa peke yake wakati wa kula; akala kila mtu peke yake? Wakasema: Ndiyo. Akasema: Basi kusanyikeni na mle pasina kutengana, na mtaje jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula kwa kusema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mtabarikiwa ndani yake na mtashiba.
Mafunzo: Basi kusanyikeni katika chakula chenu, na mkitajie jina…
- Kukusanyika kwa ajili ya chakula na kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula ni sababu ya kupata baraka katika chakula, na kupatikana shibe kwa kukila kwake.
- Utengano wote ni shari, na umoja wote ni heri.
- Himizo la kukusanyika na kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa chakula.
- Amesema Assanadi: Kwa sababu ya mkusanyika baraka huteremka katika chakula, na kwa kulitaja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu Shetani hushindwa kukifikia chakula.
Makundi :
Adabu za kisheria.
· Adabu za kula na kunywa.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
الله أكبر
Allah est le plus grand