Islam > Sw > Hadith > Quran tukufu na elimu zake > Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapolala kitandani kwake wakati wa kil…
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا أَوَى إِلَى فِرَاشِهِ كُلَّ لَيْلَةٍ جَمَعَ كَفَّيْهِ، ثُمَّ نَفَثَ فِيهِمَا فَقَرَأَ فِيهِمَا: {قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ}، وَ{قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ}، وَ{قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ}، ثُمَّ يَمْسَحُ بِهِمَا مَا اسْتَطَاعَ مِنْ جَسَدِهِ، يَبْدَأُ بِهِمَا عَلَى رَأْسِهِ وَوَجْهِهِ وَمَا أَقْبَلَ مِنْ جَسَدِهِ، يَفْعَلُ ذَلِكَ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ.
Ilikuwa katika miongozo yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- pindi anapopanda kitandani kwake kwa ajili ya kulala, ni kukusanya viganja vyake na kuviinua juu kama anavyofanya mwenye kuomba-na huvipuliza viganja hivyo kwa mdomo wake upulizaji wa taratibu pamoja na kutemea matemate kidogo na anasoma Sura tatu {Qul-huwallahu Ahadu} na {Qul-audhu birabbil falaq} na {Qul-auudhu birabbi naas} Kisha hupaka kwa kutumia viganja vyake sehemu anayoweza katika mwili wake; Kwa kuanzia kichwa chake na uso wake na sehemu ya mbele katika mwili wake, na hurudia kitendo hicho mara tatu.
Makundi : Qur'an tukufu na Elimu zake · Fadhila za Qur'an. · Adabu za kisheria. · Adabu za kulala na Kuamka. · Fadhila za Sura na Aya. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.