Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Atakapotawadha mmoja wenu basi na aweke maji puani mwake kisha ayapenge, na atakayestanji …
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureAmebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baadhi ya hukumu za twahara, miongoni mwake: Ya kwanza: Nikuwa mwenye kutawadha ni lazima aingize maji puani mwake kwa kuyavuta kwa pumzi, kisha ayatoe kwa pumzi pia. Ya pili: Nikuwa atakayetaka kusafisha udhia uliomtoka na kuuondoa pasina kutumia maji kama kwa jiwe na mfano wake, basi kusafisha kwake kuwe kwa idadi ya mamoja (witiri) kwa uchache tatu na kuendelea yatakayoweza kutakatisha kilichotoka na kusafisha mahali. Ya tatu: Kuwa atakayeamka kutoka katika usingizi wa usiku asiingize kiganja chake ndani ya chombo ili atawadhe mpaka akioshe mara tatu nje ya chombo, kwani hajui ni mahali gani ulilala mkono wake, hauwezi kuaminika na kutokuwa na najisi, na huenda shetani aliuchezea na akaubebesha vitu vyenye kumdhuru mwanadamu au vyenye kuharibu maji.
Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Twahara - usafi- · Adabu za kisheria. · Adabu za kulala na Kuamka. · Fiq'hi na misingi yake. · Adabu za Kukidhi Haja. · Udhu - kutawadha. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.