Atakapoota mmoja wenu ndoto anayoipenda basi ndoto hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo,…
Islam > Sw > Hadith > Adabu za kisheria > Atakapoota mmoja wenu ndoto anayoipenda basi ndoto hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo,…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Atakapoota mmoja wenu ndoto anayoipenda basi ndoto hiyo…
Maelezo ya hadith: Atakapoota mmoja wenu ndoto anayoipenda basi ndoto hiyo…
Ameeleza Mtume rehema amani ziwe juu yake kuwa ndoto njema yenye kufurahisha usingizini hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na akaeleza amshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo, na akiota yanayomchukiza na kumhuzunisha basi hayo yanatokana na Shetani; aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake, na wala asimsimulie yeyote; kwani ndoto hiyo haitomdhuru, kwani Mwenyezi Mungu ameyafanya hayo yaliyotajwa kuwa ni sababu ya kusalimika na kero zinazoambatana na ndoto.
Mafunzo: Atakapoota mmoja wenu ndoto anayoipenda basi ndoto hiyo…
- Migawanyiko ya ndoto: 1- Ndoto njema, nayo ni ndoto ya kweli na ni habari njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu anayoiona mtu au ikaonwa na mtu mwingine. 2- Mawazo: Nayo ni yale ambayo mtu huwaza mwenyewe akiwa macho. 3- Kutiwa huzuni na hofu na Shetani na vitisho kutoka kwake ili amuhuzunishe mwanadam.
- Uhalisia wa haya yaliyotajwa katika mlango wa ndoto njema ni mambo matatu: Amshukuru Mwenyezi Mungu juu ya ndoto hiyo, na ajipe habari njema, na aihadithie, lakini asimueleze ila yule anayempenda nasi anayemchukia.
- Na uhalisia wa hayo yaliyotajwa katika adabu za ndoto zenye kuchukiza ni mambo matano: Ajikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake, na kutokana na shari ya Shetani, na ateme kushoto mara tatu pale anaposhituka kutoka usingizini mwake, na wala asiisimulie kamwe kwa yeyote, na anapotaka kurejea katika usingizi wake basi ageukie ubavu mwingine tofauti na ule aliokuwa mwanzo; kwani ndoto hiyo wala haitomdhuru.
- Amesema bin Hajari: Hekima na lengo la kukatazwa kumsimulia asiyempenda nikuwa endapo atamsimulia huenda akamfasiria kwa mambo yenye kumchukiza, ima kwa sababu ya chuki au husuda, na huenda ikatokea kwa namna ile ile aliyomfasiria au akajiwahi mwenyewe kwa kuanza kuhuzunika na kukosa furaha, akaamrisha kuacha kumhadithia asiyempenda kwa sababu hiyo.
- Kushukuru pale zinapotokea neema, na kujirudiarudia kwa mazuri, hilo ni sababu ya kuyadumisha mazuri hayo.
Makundi :
Adabu za kisheria.
· Adabu za kuona Ndoto
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
سبحان الله وبحمده
Gloire et louange à Allah