Msiwaanze Mayahudi wala wakristo kwa salam, mkikutana na mmoja wao njiani basi mbaneni mpa…
Islam > Sw > Hadith > Adabu za kisheria > Msiwaanze Mayahudi wala wakristo kwa salam, mkikutana na mmoja wao njiani basi mbaneni mpa…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Msiwaanze Mayahudi wala wakristo kwa salam, mkikutana n…
Maelezo ya hadith: Msiwaanze Mayahudi wala wakristo kwa salam, mkikutana n…
Anakataza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwaanza Mayahudi na Wakristo kwa salam, hata kama watakuwa wamepewa hifadhi katika nchi za kiislamu, achilia mbali makafiri wengineo, na akabainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa tutakapokutana na mmoja wao njiani tumbane mahala pembamba, muumini ndiye atembee katikati ya njia, na anayepisha ni kafiri, na muislamu asiwe dhalili kwa hali yoyote ile.
Mafunzo: Msiwaanze Mayahudi wala wakristo kwa salam, mkikutana n…
- Haitakiwi kwa muislamu kumuanza yeyote katika Mayahudi na Wakristo kwa salam, na makafiri wengineo.
- Inafaa kujibu salam zao wao watakapoanza kutoa salam kwa kusema: Na kwenu pia.
- Haitakiwi kwa muislamu kukusudia kumuudhi kafiri kwa kumbana kwa makusudi pasina sababu; ili amsukumie mahala pafinyu pa njia; lakini njia ikiwa nyembamba au inamsongamano basi muislamu ndiye mwenye haki zaidi, na kafiri ndiye apishe.
- Kudhihirisha utukufu wa waislamu na unyonge wa wasiokuwa wao, pasina kuwadhulumu au kuwaambia maneno machafu.
- Kuwabana makafiri ni kwa sababu ya ukafiri walionao wa kumkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, huenda hilo likawa sababu ya kusilimu; akasalimika na moto, ikiwa hilo litawafanya kujua sababu ya kufanyiwa hivyo.
- Hakuna ubaya kwa muislamu kumwambia kafiri mwanzo wa mazungumzo, vipi hali yako?, Umeamkaje? Umeshindaje? Ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo; kwa sababu katazo hapa linachukuliwa ni katika salam ya kiislamu.
- Amesema Attwayibi: Kauli iliyopendekezwa nikuwa mtu wa bida haanzwi kwa salam, na akimsalimia asiyemjua kisha akabaini kuwa si muislamu asema: Nimerudisha salam yangu, kama kumdharau.
Makundi :
Adabu za kisheria.
· Adabu za kutoa salamu na kubisha Hodi.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا إله إلا الله
Pas de divinité sauf Allah