Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Atakayesema: -Yaani: anapotoka nyumbani kwake-: Bismillaahi tawakkaltu a'la llaahi -kwa ji…
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعن أنس بن مالك رضي الله عنه مرفوعًا: «من قال -يعني: إذا خَرج من بَيتِه-: بِسم الله تَوَكَّلتُ على اللهِ، وَلاَ حول ولا قُوَّة إِلَّا بالله، يُقَال له: هُدِيتَ وَكُفِيتَ وَوُقِيتَ، وَتَنَحَّى عَنه الشَّيطَان».
زاد أبو داود: «فيقول -يعني: الشيطان- لِشَيطان آخر: كَيف لَك بِرَجلٍ قَد هُدِيَ وكُفِيَ ووُقِيَ؟».
Ameeleza Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa mtu atakapotoka nyumbani kwake na akasema: Bismillaahi -kwa jina la Mwenyezi Mungu-, Tawakkalu a'lallaahi -Nimemtegemea Mwenyezi Mungu-, Laa haulaa walaa quwwata illaa billaahi- hakuna ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, Malaika humuita Ewe mja wa Mwenyezi Mungu umeongozwa katika njia ya haki, na umetoshelezwa mahitajio yako, na umehifadhiwa dhidi ya maadui; basi shetani aliyewakilishwa kwake hujitenga mbali naye, na hapo husema shetani mwingine kumwambia shetani huyu: utawezaje kumpoteza mtu tayari kaongozwa, na katoshelezwa, na amekingwa na mashetani wote? kwasababu yeye amesema maneno haya basi wewe hutomuweza.
Makundi : Fiq'hi -Elimu- ya Dua na Dhikri mbali mbali. · Adh-kaar za kutoka na kuingia nyumbani. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.