Hawajawahi kukaa watu kikao chochote wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu ndani yake, na wala…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi elimu ya dua na dhikri mbali mbali > Hawajawahi kukaa watu kikao chochote wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu ndani yake, na wala…
Hadith imesimuliwa na: ImepokAbu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Hawajawahi kukaa watu kikao chochote wakawa hawakumtaja…
Maelezo ya hadith: Hawajawahi kukaa watu kikao chochote wakawa hawakumtaja…
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kughafilika kumtaja Mwenyezi Mungu, nakuwa hawatokaa watu katika kikao chochote na wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, na wakawa hawakumsalia Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake isipokuwa kikao hicho kitakuwa ni hasara na majuto juu yao na mapungufu siku ya Kiyama, akitaka atawaadhibu kwa madhambi yao yaliyotangulia na uzembe wao uliofuata, na akitaka atawasamehe ikiwa ni fadhila na rehema kutoka kwake.
Mafunzo: Hawajawahi kukaa watu kikao chochote wakawa hawakumtaja…
- Himizo la kufanya dhikiri na fadhila zake.
- Fadhila za vikao ambavyo anatajwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, na kumtaja Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, nakwamba vikao ambavyo havina hayo ni vikao vibaya kwa watu siku ya Kiyama.
- Tahadhari iliyotajwa ya kughafilika kumtaja Mwenyezi Mungu haishii katika vikao pekee, bali inaenea katika sehemu zingine, amesema Nawawi: Ni machukizo kwa atakayekaa mahali aondoke bila kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake.
- Masikitiko yatakayotokea siku ya Kiyama: Ima ni kwa sababu ya kupoteza malipo na thawabu kwa kutofaidika na wakati kwa kumtii Mwenyezi Mungu, na ima ni kwa madhambi na adhabu kwa kuutumia wakati kwa kumuasi Mwenyezi Mungu.
- Tahadhari hii ni pale kughafilika kutakapokuwa ni kwa mambo ya halali, je, ni vipi vikiwa vikao vya haramu ambavyo ndani yake kuna utesi na usengenyaji na mengineyo?!.
Makundi :
Fiq'hi -Elimu- ya Dua na Dhikri mbali mbali.
· Adh-kaar zote - mbalimbali.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
الحمد لله
Louange à Allah