Hassan na Hussein ni mabosi wa vijana wa peponi
Islam > Sw > Hadith > Ubora wa ahlu baiti watu wa nyumba ya mtume > Hassan na Hussein ni mabosi wa vijana wa peponi
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Hassan na Hussein ni mabosi wa vijana wa peponi
Maelezo ya hadith: Hassan na Hussein ni mabosi wa vijana wa peponi
Alieleza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kuwa wajukuu zake Hassan na Hussein watoto wa Ally bin Abii Twalib na Fatma binti wa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake na Allah amridhie, wao ni mabosi katika fadhila wa kila aliyekufa akiwa kijana na akaingia peponi, au wao ni mabosi wa vijana wa watu wa peponi, kasoro Manabii na Mahalifa (viongozi) waongofu.
Mafunzo: Hassan na Hussein ni mabosi wa vijana wa peponi
- Hapa kuna fadhila za wazi za Hassan na Hussein radhi za Allah ziwe juu yao.
- Imesemekana katika maana ya hadithi kuwa: Wao wakati wa kuzungumzwa hadithi hii walikuwa ndio mabosi wa vijana wa wale miongoni mwao watakaokuwa katika watu wa peponi katika vijana wa zama hizi, au wao ni bora kuliko yule ambaye fadhila zake hazijathibiti kwa ujumla kama Manabii na Mahalifa (viongozi), au wao ni mabosi wa kila mwenye kusifika na sifa ya ujana, kama murua (heshima) na ukarimu na ushujaa, na haukutajwa umri maalumu wa ujana; kwa sababu Hassan na Hussein walikufa wakiwa watu wazima.
Makundi :
Ubora wa Ahlu Baiti- watu wa nyumba ya mtume.
· Akida- Itikadi-
· Watu wa Nyumba.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
الله أكبر
Allah est le plus grand