Katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:- "Na wakasema msiwaache waungu wenu, wala msimuach…
Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:- "Na wakasema msiwaache waungu wenu, wala msimuach…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:- "Na wakasema m…
عن ابن عباس رضي الله عنهما في قول الله تعالى : (وَقَالُوا لا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلا سُوَاعًا وَلا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا) قال: "هذه أسماء رجال صالحين من قوم نوح، فلما هَلَكوا أَوحى الشَّيطان إلى قَومِهِم أنِ انْصِبُوا إلى مَجَالِسِهِم الَّتي كانوا يَجْلِسون فيها أنصَابًا، وسَمُّوها بأسمَائِهِم، فَفَعَلُوا، ولم تُعْبَد، حتَّى إِذَا هَلَك أُولئك ونُسِيَ العلم عُبِدت".
Maelezo ya hadith: Katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:- "Na wakasema m…
Ana tafsiri Ibn Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Aya hii tukufu kuwa miungu hii ambayo ameitaja Mwenyezi Mungu Mtukufu- Kuwa watu wa Nuhu waliusiana kuendelea kuiabudu baada ya kuwa amewakataza Nabii wao Nuhu ziwe juu yake sala na salamu- kutomshirikisha Mwenyezi Mungu- kuwa majina hayo asili yake ni majina ya watu wema miongoni mwao, walichupa mipaka ndani yake kwa ushawishi wa Ibilisi kwao mpaka wakatundika picha zao, Basi jambo likakuwa katika picha hizi mpaka yakawa masanamu yanaabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu.
Mafunzo: Katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:- "Na wakasema m…
- Nikuwa kuchupa mipaka kwa watu wema ni sababu ya kuwabudu kinyume na Mwenyezi Mungu na kuiacha dini moja kwa moja.
- Tahadhari ya kupiga picha na kutundika picha, hasa hasa picha za waheshimiwa.
- Tahadhari kutokana na vitimbi vya shetani na kuileta kwake batili katika sura ya haki.
- Tahadhari kutokana na uzushi na mambo ya kuzua hata kama lengo la mfanyaji litakuwa zuri.
- Nikuwa kupiga picha ni katika nyenzo zinazopelekea katika shirki, hivyo ni lazima kutahadhari kupiga picha za viumbe vyenye roho.
- Kujua thamani ya uwepo wa elimu na madhara ya kukosekana kwake.
- Nikuwa sababu ya kukosekana kwa elimu ni kufa wanachuoni.
- Kutahadhari na kuiga, nakuwa hilo linaweza kumpelekea mfanyaji wake katika kutoka katika Uislamu.
- Kutangulia shirki katika umma zilizotangulia.
- Nikuwa majina haya matano yaliyotajwa ni katika viabudiwa vya watu wa Nuhu.
- Kubainishwa kubebana na kusaidiana watu wa batili juu ya batili yao.
- Kufaa kuwaombea mabaya makafiri kwa njia ya ujumla.
Makundi :
Akida- Itikadi-
· Majina na Hukumu.
· Ushirikina.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
الحمد لله
Louange à Allah