Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Atasogezwa muumini siku ya Kiyama karibu na Mola wake Mlezi Aliyetakasika na Kutukuka, kis…
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Mwenyezi Mungu kunong'ona na mja wake muumini siku ya Kiyama, akasema:
Atasogezwa muumini siku ya Kiyama karibu na Mola wake Mlezi kisha atamuwekea pazia lake la kumkinga na watu walioko katika kisimamo, hakuna atakayeona katika pazia hilo zaidi yake, hapo atamwambia:
Je walijua dhambi fulani na fulani... atamtaka akiri madhambi yake yaliyokuwa kati ya mja na Mola wake Mlezi.
Naye atasema: Ndiyo, ewe Mola Mlezi.
Mpaka atakapofadhaika muumini na kuogopa, Mtukufu atamwambia: Mimi niliyasitiri kwako madhambi haya duniani, na mimi leo hii ninayasamehe kwa ajili yako, hapo atapewa faili la mema yake.
Na ama kafiri na mnafiki wataitwa mbele ya kadamnasi: Hawa ndiyo waliomkadhibisha Mola wao Mlezi, basi tambueni kuwa laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya madhalimu.
Makundi : Akida- Itikadi- · Kuamini siku ya mwisho