Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na ka…

Islam > Sw > Hadith > Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha > Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na ka…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi…

Maelezo ya hadith: Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi…

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muumini ni mtu wa kheri maisha yake yote, lakini muumini mwenye nguvu katika imani yake na maamuzi yake na mali yake na mengineyo yenye kuendana na nguvu huyu ni bora zaidi na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko muumini dhaifu. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuusia muumini kuchukuwa sababu katika yale yenye kumnufaisha katika mambo ya Dunia na Akhera, ikiwa ni pamoja kuegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutaka msaada kwake, na kutegemea kwake. Kisha akakataza rehema na amani ziwe juu yake kuhusu kushindwa, na uvivu, na uzembe wa mtu kufanya yale yenye manufaa Duniani na Akhera. Muumini akijitahidi katika matendo, na akachukua sababu, huku akitaka msaada kwa Mwenyezi Mungu, na kwa kutaka kheri kutoka kwa Mwenyezi Mungu, basi hapo hana la kufanya zaidi ya kukabidhi jambo lake lote kwa Mwenyezi Mungu, na ajue kuwa uchaguzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndio wenye kheri, ukimpata msiba baada ya hapo, basi asiseme: "Laiti ningelifanya kadha wa kadha"; "Kwani neno "Lau" Hufungua kazi ya Shetani" kuanzia kupingana na mipango ya Allah, na kuhuzunika kwa yale aliyoyakosa, bali anatakiwa aseme tena kwa kujisalimisha na kuridhika: "Ni mipango ya Mwenyezi Mungu na alitakalo hufanya", kilichotokea ni kwa mujibu wa yale aliyoyataka Mwenyezi Mungu, kwani yeye ni mfanyaji asiye na mipaka wa yale ayatakayo, na hakuna awezaye kuzuia maamuzi yake, na hakuna awezaye kuhukumu baada ya hukumu yake.

Mafunzo: Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi…

Makundi : Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Akida- Itikadi- · Matendo ya moyoni. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima. · Ni kuamini hukumu na mipango · Mambo yanayohusu Hukumu na Mipango.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56