Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Kwa hakika Mwenyezi Mungu hamdhulumu muumini kwa jema alilofanya, huandikiwa thawabu za we…
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللهَ لَا يَظْلِمُ مُؤْمِنًا حَسَنَةً، يُعْطَى بِهَا فِي الدُّنْيَا وَيُجْزَى بِهَا فِي الْآخِرَةِ، وَأَمَّا الْكَافِرُ فَيُطْعَمُ بِحَسَنَاتِ مَا عَمِلَ بِهَا لِلَّهِ فِي الدُّنْيَا، حَتَّى إِذَا أَفْضَى إِلَى الْآخِرَةِ، لَمْ تَكُنْ لَهُ حَسَنَةٌ يُجْزَى بِهَا».
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ukubwa wa fadhila za Mwenyezi Mungu kwa waumini, na uadilifu wake kwa makafiri. Ama muumini hazipungui thawabu za mema aliyoyafanya; Bali hulipwa hapa duniani wema kwa utiifu wake, pamoja na kulimbikiziwa malipo yake huko Akhera; Na huenda akahifadhiwa malipo yake yote huko Akhera. Ama kafiri, Mwenyezi Mungu humlipa malipo kutokana na wema alioufanya kwa malipo ya mambo yaliyo mazuri hapa Duniani, mpaka inakuwa akifika Akhera, anakuwa hana thawabu na malipo atakayo lipwa huko, kwa sababu matendo mema ambayo yatamfaa hapa Duniani na Akhera lazima awe mtendaji wake ni muumini.
Makundi : Akida- Itikadi- · Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka · Kuamini siku ya mwisho · Majina na Hukumu. · Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake. · Maisha ya Akhera. · Uislamu