Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Moto wenu wa Dunia ni sawa na sehemu tu ya sabini itokanayo na moto wa Jahannam
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «نَارُكُمْ جُزْءٌ مِنْ سَبْعِينَ جُزْءًا مِنْ نَارِ جَهَنَّمَ»، قِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنْ كَانَتْ لَكَافِيَةً. قَالَ: «فُضِّلَتْ عَلَيْهِنَّ بِتِسْعَةٍ وَسِتِّينَ جُزْءًا كُلُّهُنَّ مِثْلُ حَرِّهَا».
Anatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Moto wa Duniani ni sehemu moja tu kutoka katika Moto wa Jahannam, Hivyo basi moto wa Akhera ukali wake unazidi Moto wa Duniani mara sitini na tisa, kila sehemu moja ya moto huo upo sawa na ukali wa moto wa Duniani. Kukasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa hakika Moto wa Duniani ulikuwa unatosha kuwaadhibu waliokuwamo humo, Akasema: Moto wa Jahannam umeuzidi moto wa Duniani kwa zaidi ya mara sitini na tisa, na mara zake zote hizo sitini na tisa ni sawa na mara moja kutokana na ukali wake.
Makundi : Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Akida- Itikadi- · Sifa za pepo na moto. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima. · Kuamini siku ya mwisho