Amekwisha ionja ladha ya imani, yule mwenye kumridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola wake,…

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Amekwisha ionja ladha ya imani, yule mwenye kumridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola wake,…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Amekwisha ionja ladha ya imani, yule mwenye kumridhia M…

Maelezo ya hadith: Amekwisha ionja ladha ya imani, yule mwenye kumridhia M…

Anaeleza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kuwa muumini mkweli katika imani yake uliyetulizana moyo wake kwa imani yake, atapata ukunjufu na wasaa na furaha ndani ya moyo wake na utam na ladha ya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu endapo ataridhia kwa mambo haya matatu:

La kwanza: Akiridhika kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wake Mlezi, na hii ni kwa kukunjuka kifua chake kwa yale yanayomfikia kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa muktadha wa ulezi, ikiwemo kugawa riziki na hali za waja, asipate upinzani kwa kitu chochote ndani ya nafsi yake, na asitafute Mola Mlezi zaidi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

La pili: Aridhie kuwa Uislamu ndio Dini ya kweli, na hii ni kwa kukunjuka kifua chake kwa yale yanayofungamana na Uislamu kama sheria na wajibu, na asipite njia nyingine isiyokuwa Uislamu.

La tatu: Aridhie kuwa Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake ni Mtume, na hii ni kwa kukunjuka kifua chake na afurahie yote aliyokuja nayo pasina kusitasita wala kutia shaka, na asipite ila njia inayokwenda sambamba na muongozo wake rehema na amani ziwe juu yake.

Mafunzo: Amekwisha ionja ladha ya imani, yule mwenye kumridhia M…

Makundi : Akida- Itikadi- · Majina na Hukumu. · Kuzidi kwa Imani na Kupungua kwake.

بسم الله الرحمن الرحيم mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
أحدب متناقص Gibbeuse Décroissante Jour 17.1 / 29.5
Illumination 94%
Nouvelle lune dans 12 jours
الحمد لله Louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56