Islam > Sw > Hadith > Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha > Hakika kundi la kwanza la watu watakaoingia peponi watakuwa katika sura ya mwezi usiku wa …
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureAmeeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kundi la kwanza la waumini watakaoingia peponi nyuso zao zitakuwa na sura ya mwezi unapokuwa usiku wa tarehe kumi na tano katika mg'ao, kisha wale wanaowafuata watakuwa katika sura ya nyota kali yenye mng'ao na mwangaza katika mbingu, watakuwa na sifa za ukamilifu kiasi kwamba hawatokojoa, wala kujisaidia haja kubwa, na wala hawatotema mate wala kupenga kamasi, vitana vyao ni vya dhahabu, na jasho lao ni miski, na vitezo vyao vitakuwa vinafuka hurufu nzuri mno, na udi mzuri zaidi, na wake zao watakuwa ni Mahurulaini, umbile lao litakuwa kama umbile la mtu mmoja, watakuwa katika sura ya baba yao Adam katika urefu na umbile; ulikuwa urefu wa mwili wake ni dhiraa sitini kwenda juu.
Makundi : Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Akida- Itikadi- · Sifa za pepo na moto. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima. · Kuamini siku ya mwisho · Maisha ya Akhera.