Halitoacha kuendelea kudhihiri kundi katika Umma wangu, mpaka iwajie amri ya Mwenyezi Mung…
Islam > Sw > Hadith > Characteristics of the people of the sunnah and the community > Halitoacha kuendelea kudhihiri kundi katika Umma wangu, mpaka iwajie amri ya Mwenyezi Mung…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Halitoacha kuendelea kudhihiri kundi katika Umma wangu,…
Maelezo ya hadith: Halitoacha kuendelea kudhihiri kundi katika Umma wangu,…
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa hawatoacha watu katika Umma wake kuendelea kuwepo, na kuwashinda wanaopingana nao, na hilo litaendelea mpaka iwajie amri ya Mwenyezi Mungu kwa kuchukuliwa roho zao mwisho wa zama za dunia kabla ya kusimama kwa Kiyama.
Mafunzo: Halitoacha kuendelea kudhihiri kundi katika Umma wangu,…
- Muujiza wa wazi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwani wasifu huu bado unaendelea Alhamdulillaah, kwanzia zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake mpaka hivi sasa, na bado utaendelea mpaka ije amri ya Mwenyezi Mungu iliyotajwa katika hadithi.
- Fadhila za kuwa na msimamo katika haki na kuifanyia kazi, na himizo juu ya hilo.
- Kudhihiri kwa dini kuna aina mbili: Ima kudhihiri kwa hoja na ubainifu na uwazi, na ima kudhihiri kwa dola na mhimili, na kudhihiri kulikobakia ni kwa hoja na ubainifu; kwa sababu hoja ya Uislamu ni Qur'ani, nayo iko wazi na inavitawala vitabu vingine visivyokuwa hiyo, lakini aina ya pili ya kudhihiri, ni kudhihiri kwa nguvu ya dola na mhimili, na hii inategemea kulingana na imani na kuwa na nguvu katika ardhi.
Makundi :
Characteristics of the People of the Sunnah and the Community
· Akida- Itikadi-
· People of the Sunnah and the Community
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
حسبنا الله ونعم الوكيل
Allah nous suffit, quel excellent protecteur