Umejengwa uislamu kwa mambo matano

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Umejengwa uislamu kwa mambo matano

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Bukhari na Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Umejengwa uislamu kwa mambo matano

عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ بْنِ الخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «بُنِيَ الإِسْلَامُ عَلَى خَمْسٍ: شَهَادَةِ أَنْ لَا إلَهَ إلَّا اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا ‌عَبْدُهُ ‌وَرَسُولُهُ، وَإِقَامِ الصَّلَاةِ، وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ، وَحَجِّ الْبَيْتِ، وَصَوْمِ رَمَضَانَ».

Maelezo ya hadith: Umejengwa uislamu kwa mambo matano

Ameufananisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Uislamu na jengo madhubuti kwa nguzo zake tano zenye kulibeba jengo hilo, na mambo mengine ya Uislamu kama nyenzo zenye kulikamilisha jengo hilo, Na nguzo ya kwanza katika nguzo hizo ni: Shahada mbili; Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hizo mbili ni nguzo moja; kila moja haitengani na nyingine, mja anazitamka kwa kukiri umoja wa Mwenyezi Mungu na kustahiki kwake kuabudiwa yeye pekee pasina mwingine, na kufanyia kazi makusudio ya nguzo hii, na kwa kuamini utume wa Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kumfuata yeye. Na nguzo ya pili: Ni kusimamisha swala, nazo ni swala tano za faradhi usiku na mchana: Alfajiri, Adhuhuri, lasiri, Maghribi, na Ishaa, kwa sharti zake na nguzo zake na wajibu wake. Na nguzo ya tatu: Ni kutoa zaka ya lazima, nayo ni ibada ya mali ya wajibu katika kila mali iliyofikia kiwango maalumu katika sheria, ambayo hupewa wastahiki wake. Na nguzo ya nne: Ni Hija, nayo nikutia nia ya kwenda Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada, kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka. Na nguzo ya tano: Ni kufunga mwezi wa Ramadhani, nako ni kujizuia na kula na kunywa na vinginevyo miongoni mwa vyenye kufunguza kwa nia ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuzama jua.

Mafunzo: Umejengwa uislamu kwa mambo matano

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Sala. · Zaka. · Funga. · Hijja na Umra. · Akida- Itikadi- · Fiq'hi na misingi yake. · Wajibu wa Swala na Hukumu ya Mwenye kuiacha. · Ulazima wa Zaka na Hukumu ya Mwenye kuiwacha. · Obligation of Fasting and Ruling of Its Abandoning · Obligation of Hajj and ‘Umrah and Ruling of Its Abandoner · Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka · Kuamini mitume · Majina na Hukumu. · Utume. · Uislamu

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
الله أكبر Allah est le plus grand

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56