Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya ushirikina

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya ushirikina

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Ahmad

Ni nzuri (Hasan)

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya ushirikina

عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ الْجُهَنِيِّ رضي الله عنه: أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَقْبَلَ إِلَيْهِ رَهْطٌ، فَبَايَعَ تِسْعَةً وَأَمْسَكَ عَنْ وَاحِدٍ، فَقَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، بَايَعْتَ تِسْعَةً وَتَرَكْتَ هَذَا؟ قَالَ: «إِنَّ عَلَيْهِ تَمِيمَةً»، فَأَدْخَلَ يَدَهُ فَقَطَعَهَا، فَبَايَعَهُ، وَقَالَ: «مَنْ عَلَّقَ تَمِيمَةً فَقَدْ أَشْرَكَ».

Maelezo ya hadith: Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya ushirikina

Walikuja watu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na idadi yao walikuwa kumi, akawaunga mkono tisa miongoni mwao juu ya Uislamu na kufuata sheria, na hakumuunga mkono wa kumi, alipoulizwa kuhusu sababu yake, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Huyo kavaa hirizi, nayo ni kila kinachotundikwa, ikiwemo shanga na vinginevyo kwa lengo la kuzuia kijicho au madhara. Yule bwana akaingiza mkono wake mahali ilipo hirizi na akaikata na akaepukana nayo, hapo Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuunga mkono, na akasema akitahadharisha kuhusu hirizi na akibainisha hukumu yake: "Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya shirki".

Mafunzo: Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya ushirikina

Makundi : Akida- Itikadi- · Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka · Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.

بسم الله الرحمن الرحيم mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
أحدب متناقص Gibbeuse Décroissante Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
أستغفر الله Je demande pardon à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56