“Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Motoni wenye adhabu nafuu zaidi siku ya Kiyama:…
Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > “Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Motoni wenye adhabu nafuu zaidi siku ya Kiyama:…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: “Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Motoni wenye…
Maelezo ya hadith: “Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Motoni wenye…
Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameeleza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu ambao watateswa kidogo na Moto wa Jahannam baada ya kuingia humo: Lau mngekuwa na dunia na vyote vilivyomo ndani yake, mngeweza kujikomboa kutokana na mateso haya? Watasema: Ndio, Basi Mwenyezi Mungu atasema: Nilikutaka na nikakuamrisheni jambo jepesi kuliko hilo, ilipo chukuliwa ahadi kwenu mkiwa katika mgongo wa Adam, ya kwamba msinishirikishe na chochote. Nilipowatoa katika dunia hii mlikataa kufanya chochote isipokuwa ushirikina.
Mafunzo: “Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia watu wa Motoni wenye…
- Thamani ya tauhidi na wepesi wa kuifanyia kazi.
- Hatari ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kitu kingine na mwisho wake mbaya.
- Mwenyezi Mungu alichukua ahadi kwa wanadam wote wakiwa katika mgongo wa baba yao Adam ya kutomshirikisha.
- Tahadhari ya ushirikina nakuwa thamani ya dunia yote haiwezi kumsaidia chochote kafiri siku ya Kiyama.
Makundi :
Akida- Itikadi-
· Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka
· Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
سبحان الله وبحمده
Gloire et louange à Allah