Islam > Sw > Hadith > 7 kuamrisha mema na kukataza mabaya > Hakika watu wakimuona dhalimu na wasimchukulie hatua, basi wako karibu Mwenyezi Mungu kuwa…
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureAnasimulia Abubakari Swiddiq, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, kuwa watu wanasoma aya hii:
"Enyi mlioamini lililo lazima juu yenu ni nafsi zenu hatokudhuruni aliyepotoka ikiwa mtaongoka" [Maaida: 105]
Na wanaielewa kuwa mtu anatakiwa ajitume kuirekebisha nafsi yake pekee, na kwamba hatodhurika baada ya hapo kwa upotofu wa wale waliopotea, na kuwa hawajaamrishwa kuamrisha mema na kukataza maovu!
Basi akawajulisha kuwa haikuwa hivyo, na kwamba alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Iwapo watu watamuona dhalimu na wasimzuie na dhulma yake, na hali yakuwa wana uwezo wa kumzuia, basi Mwenyezi Mungu yuko karibu kueneza adhabu kutoka kwake kwa wote, anayefanya uovu na anayenyamaza juu yake.
Makundi : 7- Kuamrisha Mema Na Kukataza Mabaya: · 7- Hukumu ya kuamrisha Mema Na Kukataza Mabaya: · Da'awa na (kujitolea) kuamrisha mema na kukataza mabaya