Hakika dini ni nyepesi, na hatoifanyia mkazo dini yeyote ila itamshinda, basi shikamaneni …

Islam > Sw > Hadith > Kulingania na kuelekeza kwa mungu > Hakika dini ni nyepesi, na hatoifanyia mkazo dini yeyote ila itamshinda, basi shikamaneni …

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Hakika dini ni nyepesi, na hatoifanyia mkazo dini yeyot…

Maelezo ya hadith: Hakika dini ni nyepesi, na hatoifanyia mkazo dini yeyot…

Alibainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Dini ya Uislamu imeegemezwa katika usahilishaji na wepesi katika mambo yake yote, na usahilishaji unathibitishwa pale panapotokea sababu ya kutokuwa na uwezo na haja, kwa sababu kuzama ndani sana katika matendo ya dini na kuacha upole matokeo yake ni kutoweza na kukoma kufanya amali zote au baadhi yake. Kisha akahimiza rehema na amani ziwe juu yake kuwa kati na kati pasina kupitiliza; Mja asifanye uzembe katika yale aliyoamrishwa, na wala asijibebeshe asiyoyaweza, akishindwa kuifanya amali nzima kamili; basi afanye inayokaribiana na hiyo.

Alitoa habari njema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya malipo makubwa ya amali ya kudumu, hata ikiwa ni kidogo, kwa wale ambao hawawezi kufanya amali nzima kikamilifu, kwa sababu ikiwa kushindwa huko hakutokani na yeye mwenyewe, hakutopelekea kupunguzwa kwa malipo yake.

Na kwa kuwa ulimwengu huu kwa hakika ni mahala pa kusafiri na mapito ya kuelekea Akhera, ameamrisha rehema na amani ziwe juu yake kutaka msaada katika kudumisha ibada kwa kuiweka nyakati tatu ambazo mtu anakuwa na hamasa:

Wakati wa kwanza ni Asubuhi: Kwa kwenda mwanzo wa mchana; kati ya swala ya Alfajiri na kuchomoza jua.

Wa pili: Mchana: Kwa kwenda wakati linapopinduka jua.

Wa tatu: Giza: kwa mwendo wa usiku mzima au sehemu yake, na kwa sababu amali ya usiku ni ngumu zaidi kuliko amali ya mchana, akaamrisha kufanya baadhi yake, kwa kauli yake: Na baadhi ya usiku.

Mafunzo: Hakika dini ni nyepesi, na hatoifanyia mkazo dini yeyot…

Makundi : Kulingania na kuelekeza kwa Mungu. · Ubora wa uislamu na uzuri wake. · Da'awa na (kujitolea) kuamrisha mema na kukataza mabaya

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
حسبنا الله ونعم الوكيل Allah nous suffit, quel excellent protecteur

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56