Islam > Sw > Hadith > Siasa ya kisheria > Laiti wangeingia wasingelitoka humo mpaka siku ya Kiyama; Utiifu unakuwa katika jambo jema
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureAlituma Jeshi Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akamfanya bwana mmoja katika Maanswari kuwa kiongozi wao, na akawaamrisha wamtii, yule kiongozi akawakasirikia na akasema kuwaambia: Hivi hakuwaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mnitii? Wakasema: Hasa! akasema: Basi nimekuamrisheni nikusanyieni kuni na muwashe moto kisha muingie humo, wakakusanya kuni na wakawasha moto, walipotaka kuingia humo, wakaanza kutazamana wao kwa wao. Na wakasema: Hakika sisi hatukumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake ila ni kwa sababu ya kuukimbia moto, je, tuuingie? wakiwa bado wako katika hali hiyo muwako wa moto ukazimika, na ikatoweka kwa kiongozi ghadhabu yake. Akaelezwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hilo akasema: Lau wangelimtii na wakaingia katika moto waliouwasha basi wangeliadhibiwa humo na wasingetoka kamwe kwa muda wa kubakia dunia, hakuna kumtii kiumbe katika kumuasi muumba; bali utiifu ni wajibu katika mambo mema na si katika maasi.
Makundi : Siasa ya Kisheria. · Njia za kumchagua Imamu kwa ajili ya uongozi mkuu · Historia ya Mtume. · Vita alivyoshiriki na Ambavyo hajashiriki Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake: · Da'awa na (kujitolea) kuamrisha mema na kukataza mabaya · Historia na Taarekh.