Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Bukhari na Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi

عَنْ أَبِي عَبْدِ اللَّهِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم يَقُولُ: «إنَّ الحَلَالَ بَيِّنٌ، وَإِنَّ الحَرَامَ بَيِّنٌ، وَبَيْنَهُمَا مُشْتَبِهَاتٌ لَا يَعْلَمُهُنَّ كَثِيرٌ مِنَ النَّاسِ، فَمَنْ اتَّقَى الشُّبُهَاتِ اسْتَبْرَأَ لِدِينِهِ وَعِرْضِهِ، وَمَنْ وَقَعَ فِي الشُّبُهَاتِ وَقَعَ فِي الحَرَامِ، كَالرَّاعِي يَرْعَى حَوْلَ الحِمَى يُوشِكُ أَنْ يَرْتَعَ فِيهِ، أَلَا وَإِنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمًى، أَلَّا وَإِنَّ حِمَى اللَّهِ مَحَارِمُهُ، أَلَّا وَإِنَّ فِي الجَسَدِ مُضْغَةً إذَا صَلَحَتْ صَلَحَ الجَسَدُ كُلُّهُ، وَإذَا فَسَدَتْ فَسَدَ الجَسَدُ كُلُّهُ، أَلَا وَهِيَ القَلْبُ».

Maelezo ya hadith: Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kanuni kuu katika mambo, nakuwa zinagawanyika sehemu tatu katika sheria: Halali ya wazi, na haramu ya wazi, na mambo yenye kutatiza, hukumu yake haiko wazi upande wa uhalali na uharamu, watu wengi hawajui hukumu yake.

Atakayeacha mambo hayo yenye kutatiza kwake, dini yake itasalimika kwa kuwa mbali na kuingia katika haramu, na heshima yake itasalimika kutokana na maneno ya watu, kwa yale wanayoweza kumuaibisha kwa kuyafanya kwake haya yenye kutatiza. Na asiyeyaepuka yenye kutatiza atakuwa kaitumbukiza nafsi yake, ima katika haramu, au watu kumkosea heshima yake. Na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kapiga mfano ili abainishe hali ya mwenye kuyafanya mambo yenye kutatiza, nakuwa yeye ni sawa na mchunga mifugo, mwenye kuchunga karibu na ardhi ambayo kaihifadhi mwenye ardhi hiyo, inahofiwa mifugo yake kulisha katika mipaka hii kwa sababu ya ukaribu wake, na hivyo hivyo mwenye kufanya mambo yenye utata ndani yake, basi kwa kufanya hivyo anakuwa karibu na haramu na anahofiwa kutumbukia ndani yake. Na baada yake akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama (Nacho ni moyo) mwili hutengemaa kwa kutengemaa kwake, na huharibika kwa kuharibika kwake.

Mafunzo: Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi

Makundi : Mambo yaliyo bora. · Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Fadhila za matendo ya moyoni. · Kuzitakasa Nafsi. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
الله أكبر Allah est le plus grand

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56