Ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni swala kwa wakati wake", A…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni swala kwa wakati wake", A…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Aka…

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بِن مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: سَأَلْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَيُّ العَمَلِ أَحَبُّ إِلَى اللَّهِ؟ قَالَ: «الصَّلاَةُ عَلَى وَقْتِهَا»، قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «ثُمَّ بِرُّ الوَالِدَيْنِ» قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «الجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ» قَالَ: حَدَّثَنِي بِهِنَّ، وَلَوِ اسْتَزَدْتُهُ لَزَادَنِي.

Maelezo ya hadith: Ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Aka…

Aliulizwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Ni amali ipi inapendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu?. Akasema: Ni swala za faradhi katika wakati wake uliopangwa na sheria, Kisha wema kwa wazazi wawili, kwa kuwafanyia wema, na kusimamia haki zao, na kuacha kuwaasi, kisha Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kunyanyua neno la Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuitetea dini ya Uislamu na waislamu, na kudhihirisha alama zake, na hii inakuwa kwa nafsi na mali.

Akasema bin Masoud Radhi za Allah ziwe juu yake: Alinieleza amali hizi; na lau kama ningelimwambia: Kisha ipi? Basi angenizidishia.

Mafunzo: Ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Aka…

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Sala. · Mambo yaliyo bora. · Ubora na fadhila za matendo mema. · Fiq'hi na misingi yake. · Fadhila za Swala. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
اللهم صل على محمد Ô Allah prie sur Muhammad

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56