Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakuniswalia

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi elimu ya dua na dhikri mbali mbali > Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakuniswalia

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ahmad

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakun…

Maelezo ya hadith: Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakun…

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha kumtakia rehema wakati wa kusikia jina lake au wasifu wake, na akasema: Bahili kamili ni yule nitakayetajwa mbele yake na akawa hakunitakia rehema; na hili ni kwa sababu ya mambo yafuatayo:

La kwanza: Nikuwa ni ubahili kwa kitu ambacho mtu hapati hasara sawa iwe ndogo au kubwa, wala hatoi mali, na wala hatumii nguvu wala juhudi.

La pili: Ni kuifanyia ubahili nafsi yake kwa sababu anainyima malipo ya kumtakia rehema Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake: kwa sababu anapojizuia kumtakia rehema atakuwa kafanya ubahili na kakataa kutimiza haki ya wajibu kwake kuitekeleza, kwa kutekeleza amri na akapata malipo.

La tatu: Kumtakia rehema ndani yake kuna kutimiza haki za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, yeye ndiye aliyetufundisha, na yeye ndiye aliyetuelekeza, na yeye ndiye aliyetuita kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akaja na wahyi huu, na sheria hii, yeye ndiye sababu ya kuongoka kwetu baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, atakayeacha kumtakia rehema basi atakuwa kamfanyia ubahili Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake kwa kutompa haki ndogo kabisa miongoni mwa haki zake

Mafunzo: Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakun…

Makundi : Fiq'hi -Elimu- ya Dua na Dhikri mbali mbali. · Adh-kaar za mambo ya Dharura. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
أستغفر الله Je demande pardon à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56