Sema: Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiyekuwa na mshirika, Mwenyezi Mung…

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Sema: Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiyekuwa na mshirika, Mwenyezi Mung…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Sema: Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee a…

عَنْ سَعْدٍ رضي الله عنها قَالَ: جَاءَ أَعْرَابِيٌّ إِلَى رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: عَلِّمْنِي كَلَامًا أَقُولُهُ، قَالَ: «قُلْ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، اللهُ أَكْبَرُ كَبِيرًا، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثِيرًا، سُبْحَانَ اللهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ، لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ» قَالَ: فَهَؤُلَاءِ لِرَبِّي، فَمَا لِي؟ قَالَ: «قُلْ: اللهُمَّ اغْفِرْ لِي وَارْحَمْنِي وَاهْدِنِي وَارْزُقْنِي».

Maelezo ya hadith: Sema: Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee a…

Mtu mmoja miongoni mwa watu wa kijijini alimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amfundishe dhikiri atakayokuwa akiisema, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Sema: "Laa ilaaha illa llaah wahdahu laa shariika lahu" (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika wake) Ameanza kwa shahada ya tauhidi, na maana yake hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, "Allaahu Akbaru kabiira" Yaani: Mwenyezi Mungu ni mkubwa kuliko kila kitu na ni Mtukufu, "Na Alhamdulillaahi kathira" Yaani: Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu kwa wingi, kwa sifa zake na vitendo vyake na neema zake zisizohesabika, "Sub-haanallaahi rabbil Aalamiin" Yaani: Ametukuka na kutakasika na kila mapungufu, "Laa haulaa walaa quwwata illaa billaahil Azizil Hakiim" Yaani: Hakuna namna ya kugeuka kutoka hali moja kwenda hali nyingine isipokuwa kwa uweza wa Allah na msaada wake na taufiki yake, Yule bwana akasema: Maneno haya ni kwa ajili ya Mola wangu Mlezi, kwa kumtaja yeye na kumtukuza, ya kwangu mimi ya kujiombea mwenyewe yako wapi? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Sema: "Ewe Mola wangu nisamehe" Kwa kuyafuta madhambi na kuyasitiri, "Na unihurumie" Kwa kuniletea manufaa na masilahi ya dini na dunia kwangu, "Na uniongoze" Kwenda katika hali nzuri na katika njia iliyonyooka, "Na uniruzuku" Mali ya halali na siha na kila aina ya kheri na afya.

Mafunzo: Sema: Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee a…

Makundi : Fiq'hi -Elimu- ya Dua na Dhikri mbali mbali. · Muongozo wa Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake katika kuleta Adh-kaar- nyiradi. · Dua zilizopokelewa toka kwa mtume. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
حسبنا الله ونعم الوكيل Allah nous suffit, quel excellent protecteur

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56