Bwana mmoja alimuuliza Mtume Muhammad rehema na amani za Allah ziwe juu yake akiwa juu ya …
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Bwana mmoja alimuuliza Mtume Muhammad rehema na amani za Allah ziwe juu yake akiwa juu ya …
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Bwana mmoja alimuuliza Mtume Muhammad rehema na amani z…
Maelezo ya hadith: Bwana mmoja alimuuliza Mtume Muhammad rehema na amani z…
Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake naye akiwa anahutubia juu ya Mimbari: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nifundishe ni namna gani nitaswali usiku?. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Utaswali na kutoa salamu katika kila rakaa mbili, ukihofia kuchomoza kwa Afajiri basi swali rakaa moja itakufanyia kuwa witiri rakaa zingine ulizoswali, na hakika yeye rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiusia kuifanya swala ya mwisho ya usiku kuwa ni witiri.
Mafunzo: Bwana mmoja alimuuliza Mtume Muhammad rehema na amani z…
- Asili katika swala za usiku ni mtu atoe salamu katika kila rakaa mbili, nje na witiri.
- Nikuwa swala za usiku hazina idadi maalumu; kwa kuwa tamko liliachwa wazi.
- Amesema Nawawi: "Swala za usiku na mchana ni rakaa mbili mbili", hadithi hii inachukuliwa kama kubainisha kilicho bora zaidi, nayo ni atoe salamu katika kila rakaa mbili, na sawa sawa ziwe ni sunna za usiku na mchana, na ni sunna atoe salamu kwa kila rakaa mbili.
- Amesema Nawawi: Hapa kuna ushahidi kuwa sunna ni kuifanya witiri kuwa swala ya mwisho wa usiku, na kwamba wakati wake unamalizika kwa kuchomoza Alfajiri, na ndio kauli mashuhuri katika madhehebu yetu, na ndivyo lilivyosema jopo la wanachuoni.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Sala.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Swala ya Kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.
· Kisimamo cha Usiku.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
الله أكبر
Allah est le plus grand