Mkono unakatwa kwa robo Dinari na kuendelea
Islam > Sw > Hadith > Adhabu > Mkono unakatwa kwa robo Dinari na kuendelea
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Mkono unakatwa kwa robo Dinari na kuendelea
Maelezo ya hadith: Mkono unakatwa kwa robo Dinari na kuendelea
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwizi unakatwa mkono wake kwa kuiba robo Dinari ya dhahabu, na zaidi ya hapo, na kiwango chake kinalingana na kiasi cha Gramu 1.06 ya dhahabu.
Mafunzo: Mkono unakatwa kwa robo Dinari na kuendelea
- Wizi ni katika madhambi makubwa.
- Ameweka mpaka Mwenyezi Mungu Mtukufu wa adhabu ya mwizi, nayo ni kukata mkono wake, kama ilivyo katika kauli yake Mtukufu: "Na mwizi mwanaume na mwizi mwanamke basi ikateni mikono yao" [Maaida: 38], na mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake yamebainisha sharti za kukata huku.
- Makusudio ya mkono katika hadithi ni kukikata kiganja katika maungio yake kati yake na muundi wa mkono.
- Na miongoni mwa hekima katika kukata mkono wa mwizi, ni kulinda mali za watu, na kumkomesha mtu mwingine katika watu wanaofanya uadui katika mali za watu.
- Dinari ni uzito wa dhahabu, na inalingana kwa sasa na (Gramu 4.25) kwa kipimo cha 24; hivyo robo Dinari inalingana na gramu moja na kitu.
Makundi :
Adhabu.
· Adhabu ya wizi.
· Fiq'hi na misingi yake.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
الله أكبر
Allah est le plus grand