Amekataza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuswali baada ya swala ya sub-hi mpaka lic…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Amekataza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuswali baada ya swala ya sub-hi mpaka lic…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim kwa riwaya zake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Amekataza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuswali…

عن عبد الله بن عباس رضي الله عنه قال: «شَهِد عِندِي رِجَال مَرْضِيُون - وأَرْضَاهُم عِندِي عُمر- أنَّ النَبِي صلى الله عليه وسلم نَهَى عن الصَّلاة بَعد الصُّبح حتَّى تَطلُعَ الشَّمسُ، وبعد العصر حتَّى تَغرُب».
وعن أبي سعيد رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم أنه قال: «لا صَلاَة بعد الصُّبح حتَّى تَرتَفِعَ الشَّمسُ، ولا صَلاَة بعد العَصرِ حتَّى تَغِيبَ الشَّمس».

Maelezo ya hadith: Amekataza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuswali…

Amekataza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi hizi mbili kuswali baada ya swala ya sub-hi mpaka lichomoze jua na linyanyuke toka msitari wa mawingu katika mtazamo wa macho kwa kiasi cha urefu wa mshale, na hili linaweza kukadiriwa kwa dakika kadhaa, wametofautiana wanachuoni katika kiwango chake, kuanzia dakika tano (5) mpaka kumi na tano (15). Na amekataza pia kuswali baada ya swala ya laasiri mpaka litoweke jua, kabla ya adhana ya magharibi kwa dakika chache; kwasababu katika kuswali ndani ya nyakati hizi kuna kujifananisha na washirikina wale wanaoliabudu wakati wa kuchomoza kwake na kuzama kwake, na tumekatazwa kujifananisha nao katika ibada zao; kwasababu atakayejifananisha na watu fulani basi nayeye ni miongoni mwao.

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Sala. · Fiq'hi na misingi yake. · Nyakati zilizo katazwa kusali.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
لا حول ولا قوة إلا بالله Pas de force ni de puissance sauf en Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56