Ikiwa mmoja wenu atachukua kamba yake, akaleta mzigo wa kuni juu ya mgongo wake, akauuza, …
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa miamala > Ikiwa mmoja wenu atachukua kamba yake, akaleta mzigo wa kuni juu ya mgongo wake, akauuza, …
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Ikiwa mmoja wenu atachukua kamba yake, akaleta mzigo wa…
Maelezo ya hadith: Ikiwa mmoja wenu atachukua kamba yake, akaleta mzigo wa…
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu anapofanya kazi yoyote hata kama ni kuchukua kamba, akaitumia kukusanyia kuni juu ya mgongo wake, akaziuza na akapata chakula kwa hilo, au akatoa sadaka, na akajitosheleza na kutowaomba watu na akaulinda uso wake na udhalili wa kuombaomba; hilo ni bora zaidi kwake kuliko kuwaomba watu, ima wampe au wamnyime, kuwaomba watu ni udhalili, na muumini anaheshima na wala si dhalili.
Mafunzo: Ikiwa mmoja wenu atachukua kamba yake, akaleta mzigo wa…
- Himizo la kujizuia kuomba na kujitakasa na hilo.
- Himizo la kufanya kazi kwa ajili ya kupata riziki, hata kama mtu mzima atafanya kazi ndogo na ya udhalili katika macho ya watu.
- Vita ya Uislamu dhidi ya kuombaomba na kubweteka; na ndio maana umewajibisha kwenda mbio na kufanya kazi, hata kama itakuwa ngumu; kama kuchanja kuni kwa mfano.
- Si halali kuomba, mtu akiwa na uwezo wa kufanya kazi na kujitafutia riziki.
- Kumuomba kiongozi kukiwa na haja inafaa, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala wale waliokujia ili uwachukue ukasema: Sina kipando cha kukuchukueni. Tena wakarudi na macho yao yanamiminika machozi kwa huzuni ya kukosa cha kutoa." [Tauba: 92]
- Atakayedharurika kuomba na akawa dhaifu hawezi kujitafutia riziki na kuchanja kuni, basi inafaa kwake kuomba, lakini asing'ang'anie na kulazimisha, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hawang'ang'anii watu kwa kuwaomba" [Al-Baqara: 273].
- Amesema Nawawi: Hapa: Kuna himizo la kutoa sadaka, na mtu kula kwa chumo la mkono wake, na kutafuta riziki ya halali.
Makundi :
Fiq'hi - Ufahamu- wa miamala.
· Biashara.
· Fiq'hi na misingi yake.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
حسبنا الله ونعم الوكيل
Allah nous suffit, quel excellent protecteur