Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Hakika Allah na Mtume wake ameharamisha kuuza pombe, na mzoga na nguruwe na masanamu
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ عَامَ الفَتْحِ وَهُوَ بِمَكَّةَ: «إِنَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ حَرَّمَ بَيْعَ الخَمْرِ، وَالمَيْتَةِ وَالخِنْزِيرِ وَالأَصْنَامِ»، فَقِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَرَأَيْتَ شُحُومَ المَيْتَةِ، فَإِنَّهَا يُطْلَى بِهَا السُّفُنُ، وَيُدْهَنُ بِهَا الجُلُودُ، وَيَسْتَصْبِحُ بِهَا النَّاسُ؟ فَقَالَ: «لاَ، هُوَ حَرَامٌ»، ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عِنْدَ ذَلِكَ: «قَاتَلَ اللَّهُ اليَهُودَ إِنَّ اللَّهَ لَمَّا حَرَّمَ شُحُومَهَا جَمَلُوهُ، ثُمَّ بَاعُوهُ، فَأَكَلُوا ثَمَنَهُ».
Jabiri bin Abdillah Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema katika mwaka wa ufunguzi akiwa Makka: Hakika Mwenyezi Mungu na Mtume wake amekataza kuuza pombe, na mzoga na nguruwe na masanamu, wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je inajuzu kwetu kuuza mafuta ya wanyama waliokufa? Kwa sababu yanatumika kupaka boti (Mitumbwi), na ngozi na watu huwasha taa zao kwayo. Akasema: Hapana, kuyauza ni haramu, kisha akasema: Mwenyezi Mungu amewalaani Mayahudi, Mwenyezi Mungu alipowaharamishia mafuta ya wanyama, waliyayeyusha, kisha wakayauza na kula thamani yake.
Makundi : Vyakula na vinywaji. · Kilichokuwa halali na Haramu katika wanyama na Ndege. · Fiq'hi na misingi yake.