Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni zipi haki za mke wa mmoja wetu juu yake?, Akase…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu kuhusu familia > Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni zipi haki za mke wa mmoja wetu juu yake?, Akase…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad

Ni nzuri (Hasan)

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni zipi haki za…

Maelezo ya hadith: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni zipi haki za…

Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni zipi haki za mke juu ya mume wake? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akataja mambo kadhaa, miongoni mwa hayo ni:

La kwanza: Usijipendelee kwa chakula ukamuacha yeye; bali umlishe kama ulivyo kula wewe.

La pili: Usijipendelee kwa mavazi mazuri, bali umvishe utakapovaa wewe, na ukipata kipato na ukaweza.

La tatu: Usipige ila kuwe na sababu na haja ya kufanya hivyo, na akihitaji kumpiga ima kwa kumuadabisha au kwa kuacha kwake mambo ya faradhi, basi kiwe ni kipigo kisichovunja wala kujeruhi; na uso haupigwi;kwa sababu uso ndio kiungo kitukufu zaidi na kilicho wazi zaidi na kimekusanya viungo vitukufu, na viungo laini.

La nne: Usitukane au kusema: Mwenyezi Mungu auchafue uso wako; usimnasibishe yeye wala chochote katika mwili wake na ubaya ambao ni kinyume na uzuri; kwa sababu Mwenyezi Mungu ndiye aliutengeneza uso wa mwanadamu na mwili wake, na akakipa umbile zuri kila kiumbe, na kutukana umbile kunarudi katika kumtukana muumbaji, Mwenyezi Mungu atuepushe na hilo.

La tano: Usihame ila kitandani, na wala usiondoke hapo, na wala usimhamishie katika nyumba nyingine; na huenda hilo ni katika mambo yaliyozoeleka kutokea baina ya wanandoa.

Mafunzo: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni zipi haki za…

Makundi : Fiq'hi- ufahamu- kuhusu familia. · Ndoa. · Fiq'hi na misingi yake. · Maisha ya wanandoa.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
لا إله إلا الله Pas de divinité sauf Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56