Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi alipomuelekeza kwenda Yemen alimuamris…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi alipomuelekeza kwenda Yemen alimuamris…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ahmad
Ni sahihi kwa ushahidi wake mbalimbali
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi ali…
Maelezo ya hadith: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi ali…
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimtuma Muadhi bin Jabali radhi za Allah ziwe juu yake kwenda Yemen kwa ajili ya kuwafundisha watu na kuwafikishia ujumbe, na miongoni mwa yale aliyomuamrisha achukue kutoka kwa Waislamu zaka za ng'ombe zao katika kila ng'ombe thelathini achukue dume moja au ng'ombe aliyeanza kufuatana na wengine machungani; naye ni yule aliyetimiza mwaka moja, na katika kila ng'ombe arobaini achukue ng'ombe mkamilifu; naye ni yule aliyetimiza miaka miwili. Na achukue jizia (kodi) kutoka kwa watu wa kitabu, Mayahudi na Wakristo, kwa kila mwanaume aliyebalehe, Dinari, au kinacholingana na Dinari katika nguo za Yemen ziitwazo: Maafari.
Mafunzo: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi ali…
- Jizia haichukuliwi isipokuwa kwa yule aliyebalehe; kwa sababu kigezo cha mtu asiyechukuliwa kodi ni: Ni yule ambaye haitakiwi kumuua akitekwa: Kama mtoto mdogo, na mwanamke, na wengineo.
- Jizia makadirio yake yanarudi katika jitihada za kiongozi, kwa sababu zinatofautiana kulingana na kutofautiana kwa maeneo na zama, na utajiri na ufakiri, na ushahidi juu ya hilo nikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ndiye aliyetoa makadirio hayo kwa watu wa Yemen, akasema kumwambia Muadhi: "Chukua kwa kila aliyebalehe Dinari", wakati huo huo jizia iliongezeka katika makadirio ya Omari radhi za Allah ziwe juu yake wakati alipoweka kiwango kwa watu wa Sham.l
- Kutilia umuhimu ukusanyaji wa zaka, na kumuwakilisha mwenye kukusanya ni katika majukumu ya kiongozi.
- Tabii: Ni yule aliyetimiza mwaka mmoja, na akaingia mwaka wa pili, na ameitwa tabii; kwa sababu bado anamfuata mama yake.
- Dinari: Ni pesa ya dhahabu, na Dinari ya kislamu: Uzito wake ni gramu nne na robo ya dhahabu (4.25gm).
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Zaka.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Zaka ya wanyama wafugwao.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
سبحان الله
Gloire à Allah