Atakapo sema Muadhini: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema mmoja wenu: Allahu Akbar…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Atakapo sema Muadhini: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema mmoja wenu: Allahu Akbar…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Atakapo sema Muadhini: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kis…

Maelezo ya hadith: Atakapo sema Muadhini: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kis…

Adhana ni kuwatangazia watu kuwa muda wa swala umeingia, na maneno ya adhana ni maneno yaliyokusanya itikadi ya imani.

Na katika hadithi hii anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kinachotakiwa kisheria wakati wa kusikia adhana, nako msikiaji asema kama anavyosema muadhini, muadhini akisema: "Allahu Akbaru" Mwenye kusikia naye anasema: "Allahu Akbaru" ataendelea hivyo, isipokuwa katika kauli ya muadhini "Hayya alas swalaa", "Hayya alal falaah, atasema mwenye kusikia: "Laa haulaa wala quwwata illaa billaah".

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakaye rudia rudia nyuma ya muadhini kwa utakasifu kutoka moyoni mwake ataingia peponi.

Na maana ya maneno ya adhana ni: "Allahu Akbaru": Yaani: Yeye mtakasifu ni mtakasifu na ni mtukufu na ni mkubwa kuliko kila kitu.

"Ash-hadu an laa ilaaha illa llaah": Yaani: Hapana muabudiwa wa haki zaidi ya Allah.

"Ash-hadu anna Muhammadan Rasuulu llaah" Yaani: Nina kiri na nina shuhudia kwa ulimi wangu na moyo wangu, yakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alimtuma Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni wajibu kumtii.

"Hayya alas swalaa", Yaani: Njooni katika swala, na kauli ya mwenye kusikia: "Laa haulaa walaa quwwata illa billaah", Yaani hakuna ujanja wa kuvimaliza vikwazo vya ibada, wala nguvu ya kuzifanya na wala uwezo wa chochote ila ni kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

"Hayya alal falaah", Njooni katika sababu ya kufanikiwa, nako ni kufuzu kwa Pepo na kusalimika na moto.

Mafunzo: Atakapo sema Muadhini: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kis…

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Sala. · Mambo yaliyo bora. · Fadhila za Adh-kaar. · Fiq'hi na misingi yake. · Adhana na Iqama. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
الحمد لله Louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56