Atakapoingia mmoja wenu Msikitini basi amtakie rehema Mtume kisha aseme: Allaahummaf-tahli…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Atakapoingia mmoja wenu Msikitini basi amtakie rehema Mtume kisha aseme: Allaahummaf-tahli…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Ibn Majah na Alhakim
Ni nzuri (Hasan)
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Atakapoingia mmoja wenu Msikitini basi amtakie rehema M…
Maelezo ya hadith: Atakapoingia mmoja wenu Msikitini basi amtakie rehema M…
Amemuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Muislamu atakapotaka kuingia Msikitini amtakie rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kusema: Allaahumma swalli alaa Muhammadi, kisha aseme: "Ewe Mwenyezi Mungu nifungulie milango ya rehema zako". Na akitoka amtakie rehema Mtume na aseme: "Ewe Mwenyezi Mungu nikinge na shetani aliyelaaniwa", na katika riwaya nyingine ya imamu Hakim: Na aseme: "Awe Mwenyezi Mungu nilinde na Shetani aliyelaaniwa".
Mafunzo: Atakapoingia mmoja wenu Msikitini basi amtakie rehema M…
- Sunna ya kusoma dua hii wakati wa kuingia Msikitini na wakati wa kutoka.
- Dua hii ni kwa misikiti yote, hata Msikiti mtukufu wa Makka.
- Rehema zimetajwa maalumu wakati wa kuingia, na kukingwa na Shetani wakati wa kutoka: Ni kwakuwa mwenye kuingia anashughulika na kile kinachomuweka karibu na Mwenyezi Mungu na karibu na Pepo yake ikawa ni mahala pazuri pa kutaja rehema, na akitoka anakwenda katika dunia na yote yaliyomo miongoni mwa mapumbao na vyenye kushughulisha, ikawa ni sehemu nzuri ya kuomba ulinzi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuhifadhiwa kutokana na Shetani.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Sala.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Hukumu za Misikiti.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
الحمد لله
Louange à Allah