Fuatanisheni kati ya Hija na Umra, kwani huondoa umasikini na madhambi kama moto unavyoond…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Fuatanisheni kati ya Hija na Umra, kwani huondoa umasikini na madhambi kama moto unavyoond…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa naTirmidhiy na Nasai na Ahmad
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Fuatanisheni kati ya Hija na Umra, kwani huondoa umasik…
Maelezo ya hadith: Fuatanisheni kati ya Hija na Umra, kwani huondoa umasik…
Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuweka karibu kati ya kutimiza ibada ya Hija na ibada ya Umra, na kutoacha kuzitekeleza hali yakuwa kuna uwezo, kwa sababu kuzitekeleza kwake inakuwa ni sababu ya kuondoa umasikini na madhambi na athari zake ndani ya moyo, kama ambavyo mpulizo wa moto huwa sababu ya kuondoa uchafu wa chuma na vyote vinavyochanganyika nacho katika madini ambayo si chuma.
Mafunzo: Fuatanisheni kati ya Hija na Umra, kwani huondoa umasik…
- Fadhila za kufuatanisha baina ya Hija na umra na himizo katika hilo.
- Kufuatanisha kati ya Hija na Umra ni miongoni mwa sababu za utajiri na msamaha wa madhambi.
- Amesema Al-Mubaarakafuriy: (Huondoa umasikini) Yaani: Huuondosha kabisa, na hii inategemea maana zote mbili: Umasikini unaoonekana kwa kupatikana utajiri wa mkononi, na umasikini wa ndani, kwa kupata utajiri wa moyo.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Hijja na Umra.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Fadhila za Hijjah na Umra.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
أستغفر الله
Je demande pardon à Allah