Acha yanayokutia shaka na uende katika yale yasiyokutia shaka
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Acha yanayokutia shaka na uende katika yale yasiyokutia shaka
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Tirmidhiy na Nasaai
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Acha yanayokutia shaka na uende katika yale yasiyokutia…
عَنْ أَبِي مُـحَمَّدٍ الحَسَنِ بْنِ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ - سِبْطِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَرَيْحَانَتِهِ-، قَالَ: حَفِظْتُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «دَعْ مَا يَرِيبُك إلَى مَا لَا يَرِيبُكَ».
Maelezo ya hadith: Acha yanayokutia shaka na uende katika yale yasiyokutia…
Ameamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha lile linalokutia shaka ndani yake katika kauli na matendo kuwa limekatazwa au la, je ni halali au ni haramu, na ufanye yale usiyo na shaka nayo katika yale uliyo na uhakika na uzuri wake na uhalali wake.
Mafunzo: Acha yanayokutia shaka na uende katika yale yasiyokutia…
- Muislamu anatakiwa kujenga mambo yake juu ya yakini na kuacha yenye kutia shaka ndani yake, na awe na utambuzi katika dini yake.
- Katazo la kutumbukia katika matamanio mabaya.
- Ukitaka utulivu na raha achana na mambo yanayokutia shaka na kuyatupilia mbali.
- Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, pale alipowaamrisha katika mambo ambayo ndani yake kuna raha ya moyo, na akawakataza katika yale yanayotia msongo na utata.
Makundi :
Msingi wa Fiq'hi.
· Kukinzana na Kufanya kuwa ni sahihi.
· Fiq'hi na misingi yake.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
أستغفر الله
Je demande pardon à Allah