Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-ha…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-ha…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno…

عَنْ أَبِي مَالِكٍ الحَارِثِ بْنِ عَاصِمٍ الأَشْعَرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الطُّهُورُ شَطْرُ الْإِيمَانِ، وَالْحَمْدُ لِلهِ تَمْلَأُ الْمِيزَانَ، وَسُبْحَانَ اللهِ وَالْحَمْدُ لِلهِ تَمْلَآنِ -أَوْ تَمْلَأُ- مَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ، وَالصَّلَاةُ نُورٌ، وَالصَّدَقَةُ بُرْهَانٌ، وَالصَّبْرُ ضِيَاءٌ، وَالْقُرْآنُ حُجَّةٌ لَكَ أَوْ عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدُو، فَبَايِعٌ نَفْسَهُ فَمُعْتِقُهَا أَوْ مُوبِقُهَا»

Maelezo ya hadith: Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno…

Anafahamisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa twahara na usafi wa nje ambao ni udhu na kuoga ni sharti la usahihi wa swala. Na kuwa neno: "Alhamdulillah hujaza mizani" nako ni kumsifu Mwenyezi Mungu aliyetakasika na machafu, na kumsifia kwa sifa za ukamilifu zitakazopimwa siku ya kiyama na kuijaza mizani ya matendo. Na kuwa neno: "Sub-hanallah na Alhamdulillah" na maneno hayo ni kumtakasa Mwenyezi Mungu na kumsifia kwa sifa zilizokamilika na zilizotimia ambazo anastahiki sifa hizo pamoja kumpenda yeye na kumtukuza hujaza sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi. Na kuwa "Swala ni nuru" ya mja katika moyo wake, na katika uso wake na kaburini mwake na siku ya kufufuliwa kwake. Na kuwa "Sadaka ni ushahidi" Na ni dalili ya ukweli wa imani ya muumini, na tofauti yake na mnafiki ambaye huzuia kutoa sadaka kwa kuwa mnafiki haamini malipo ya kutoa sadaka. Na "kuwa subira ni mwangaza" -na subira ni kuizuia nafsi kutoku papatika na kuwa na hasira, subira ni nuru inayokuwa na joto na kuunguza, kama vile mwanga wa Jua; kwa sababu subira ni tabu kubwa inahitaji kuilazimisha nafsi na kuizuia na kile inachokipenda; hivyo haachi kuwa na mng'ao mtu mwenye subira, mwenye kuongoka na mwenye kudumu katika usahihi, nako ni kusubiri katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kutomuasi yeye, na kuwa na subira kwenye matatizo na aina mbalimbali za mambo yenye kuchukiza katika Dunia. Na kuwa "Qur'ani ni hoja kwako wewe" kwa kuisoma na kuifanyia kazi, au yaweza kuwa " Hoja dhidi yako" kwa kuiacha pasina kuifanyia kazi au kuisoma. Kisha akafahamisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakuwa watu wote huenda mbio na hutawanyika na huamka toka usingizini mwao na wanatoka kwenye majumba yao kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali miongoni mwao kuna wenyekuwa na msimamo katika kumtii Mwenyezi Mungu, hivyo anakuwa ameikomboa nafsi yake na moto, na miongoni mwao kuna mwenye kwenda kinyume na kuacha kumtii Mwenyezi Mungu na akaingia katika maasi, hivyo akaiangamiza na kuingia motoni.

Mafunzo: Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno…

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Twahara - usafi- · Fiq'hi -Elimu- ya Dua na Dhikri mbali mbali. · Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Faida za Kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu. · Kuzitakasa Nafsi. · Fiq'hi na misingi yake. · Udhu - kutawadha. · Fadhila - ubora wa kutawadha. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
الله أكبر Allah est le plus grand

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56