Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mimi nilionyeshwa kuwa nyinyi ndio we…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu kuhusu familia > Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mimi nilionyeshwa kuwa nyinyi ndio we…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mi…

Maelezo ya hadith: Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mi…

Alitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika siku ya Iddi kwenda katika uwanja wa swala, na alikuwa kawaahidi wanawake kuwa atawatengea nafasi ya kuwapa mawaidha, akaitimiza siku hizo, na akasema: Enyi kundi la wanawake toeni sadaka, na zidishe kuomba msamaha; kwani mambo mawili hayo ni katika sababu kubwa za kufutiwa madhambi, kwani mimi nilikuoneni usiku niliopandishwa mbinguni mkiwa wengi motoni.

Mwanamke mmoja miongoni mwao mwenye akili na mawazo mazuri na heshima, akasema: Kwani tuna nini sisi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu mpaka tuwe wengi motoni?

Akasema: Kwa sababu ya mambo kadhaa: Mnazidisha sana kulaani na matusi, na mnakanusha haki za waume. Kisha akawasifu kwa kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: Sijapata kuona wenye mapungufu ya akili na dini wanaoweza kuwashinda wenye mioyo salama na akili na maamuzi na uwezo wa kutunza kumbukumbu zao kuliko nyinyi.

Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ni upi upungufu wa akili na dini?

Akasema: Ama upungufu wa akili ni kuwa ushahidi wa wanawake wawili unalingana na ushahidi wa mwanaume mmoja; huu ndio upungufu wa akili, na upungufu wa dini, ni upungufu wa kufanya amali njema, kiasi ambacho mwanamke anakaa siku kadhaa haswali kwa sababu ya hedhi, na anafungua siku kadhaa za Ramadhani kwa sababu ya hedhi, na huu ndio upungufu wa dini, isipokuwa wao hawalaumiwi wala hawaandikiwi dhambi juu ya hilo; kwa sababu ni katika asili ya maumbile, kama ambavyo mwanadamu ameumbwa na asili ya kuipenda mali, na haraka katika mambo yake na ni mjinga.... na mengineyo, lakini alilitanabahisha hilo ikiwa ni tahadhari kwa wanaume wasifitinike nao.

Mafunzo: Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mi…

Makundi : Fiq'hi- ufahamu- kuhusu familia. · Hukumu za wanawake. · Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Sifa za pepo na moto. · Fiq'hi na misingi yake. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
اللهم صل على محمد Ô Allah prie sur Muhammad

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56