Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Toa ewe mwanadamu na mimi nikupe
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Toa ewe mwanadamu na mimi nikupe
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Toa ewe mwanadamu na mi…
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «قَالَ اللهُ: أَنْفِقْ يَا ابْنَ آدَمَ أُنْفِقْ عَلَيْكَ».
Maelezo ya hadith: Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Toa ewe mwanadamu na mi…
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Toa ewe mwanadamu -katika matumizi ya wajibu na ya hiyari- nikukunjulie na nikupe badala ya hicho na nikubariki ndani yake.
Mafunzo: Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Toa ewe mwanadamu na mi…
- Himizo la kutoa sadaka na kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu.
- Kutoa katika njia za heri ni miongoni mwa sababu kubwa za kupata baraka katika riziki na kuzidishwa kwake, na Mwenyezi Mungu kumpa badala mja katika kile alichokitoa.
- Hadithi hii ni katika zile anazozipokea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mola wake Mlezi, na huitwa Hadithil Qudsi au Hadithil Ilahi, nayo ni ile ambayo tamko lake na maana yake inatoka kwa Allah, isipokuwa haina upekee kama wa Qur'ani inaojipambanua nayo kwa vingine, ikiwa kisomo chake kutumika katika ibada, na kuwa twahara kabla ya kusoma, na kuwashinda watu kwa changamoto zake, na mengineyo.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Fiq'hi- ufahamu- kuhusu familia.
· Zaka.
· Matumizi.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Sadaka za kujitolea.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
حسبنا الله ونعم الوكيل
Allah nous suffit, quel excellent protecteur