Nilikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akafika katika jalala la watu fulan…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Nilikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akafika katika jalala la watu fulan…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Nilikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake…

عَنْ حُذَيْفَةَ رضي الله عنه قَالَ: كُنْتُ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَانْتَهَى إِلَى سُبَاطَةِ قَوْمٍ، فَبَالَ قَائِمًا، فَتَنَحَّيْتُ فَقَالَ: «ادْنُهْ» فَدَنَوْتُ حَتَّى قُمْتُ عِنْدَ عَقِبَيْهِ فَتَوَضَّأَ فَمَسَحَ عَلَى خُفَّيْهِ.

Maelezo ya hadith: Nilikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake…

Imepokelewa kutoka kwa Hudhaifa bin Al-Yaman kwamba alikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akataka kukidhi haja ndogo, akaingia dampo la watu fulani; Napo ni mahali ambapo takataka na uchafu unaofagiliwa kutoka majumbani hutupwa hapo, hivyo akakidhi haja ndogo akiwa kasimama, na huwa anakidhi haja ndogo akiwa kachuchumaa.

Basi Hudhaifa akajisogeza mbali naye, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Njoo karibu, basi Hudhaifa akamkaribia mpaka akasimama nyuma yake, nyuma ya miguu yake; Ili awe kama mstara kwake kutokana na watu kumtazama katika hali ile.

Kisha akatawadha, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, na wakati wa kuosha miguu yake, alitosheka kwa kupangusa juu ya soksi (Khofu) zake - nazo ni zile zinazovaliwa miguuni, zilizotengenezwa kwa ngozi nyembamba na mfano wake na zinazofunika vifundo vya miguu, na wala hakuzivua.

Mafunzo: Nilikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake…

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Twahara - usafi- · Fiq'hi na misingi yake. · Kufuta juu ya Khofu mbili au soksi mbili

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56