usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainni alaa dhikrika washukrika wahusni…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainni alaa dhikrika washukrika wahusni…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Abu Daud, Nasai na Ahmad
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ain…
Maelezo ya hadith: usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ain…
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alishika mkono wa Muadhi radhi za Allah ziwe juu yake, na akasema kumwambia: Wallahi hakika mimi ninakupenda, na ninakuusia ewe Muadhi usijekuacha kusema mwisho wa kila swala: Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie kukutaja, katika kila kauli na kitendo kinachoniweka karibu na utiifu, "na kukushukuru" kwa kutimia neema na kuzuia mabaya, "na kuzifanya vizuri ibada zako" kwa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa kumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Mafunzo: usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ain…
- Sheria ya kumueleza mtu kuwa unampenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
- Inapendeza kuomba dua hii mwisho wa kila swala ya faradhi na ya sunna.
- Katika kuomba kwa matamshi haya machache kuna mahitaji yote ya Dunia na Akhera
- Katika faida za kupendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kuusiana katika na kupeana nasaha katika mambo mema na uchamungu.
- Amesema Attwayibi: Kumtaja Mwenyezi Mungu ni utangulizi wa kukunjua kifua, na kumshukuru ni njia ya kuzilinda neema, na kuzifanya vizuri ibada ni kujiweka mbali na yote yanayomshughulisha mtu na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Sala.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Adh-kaar - zisomwazo- wakati wa swala.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا إله إلا الله
Pas de divinité sauf Allah