Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Anachokipata aliyekufa shahidi katika maumivu ya kifo, ni kama maumivu anayoyapata mmoja w…
Ni nzuriMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «مَا يَجِدُ الشَّهيد من مَسِّ القتل إلا كما يَجِدُ أَحَدُكُمْ من مَسِّ القَرْصَةِ».
Maana ya hadithi: nikuwa mtu atakapokufa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hakika yale yanayompata katika mguso wa kifo, na katika riwaya ya Daaramiy (katika maumivu ya kifo) hayahisi isipokuwa ni kama anavyohisi mmoja wetu anapong'atwa na mdudu chungu, na katika riwaya ya Daaramiy "kutokana na maumivu ya kung'atwa". Na maana yake nikuwa: Shahidi hasongwi na ukali wa maumivu ya kifo, kama ilivyo hali ya watu wengine, bali ukali anaoupata na ukamsumbua wakati wa kifo chake ni kama ule tunaoupata kwasababu ya kung'atwa na mdudu chungu, na maumivu anayosababu mdudu huyo na uharaka wa kumalizika kwake, basi wala hayahisi, Na hii ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa shahidi, kwani yeye alipoitanguliza roho yake katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kiurahisi, basi Mwenyezi Mungu akampunguzia juu yake maumivu ya kuuwawa.
Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Jihadi. · Fiq'hi na misingi yake. · Fadhila za Jihadi.