Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri kibaba cha tende, au kiba…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri kibaba cha tende, au kiba…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakat…
Maelezo ya hadith: Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakat…
Amewajibisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri baada ya Ramadhani, nayo kwa kiwango cha kibaba inafikia uzito wake machoto manne. Na mudi moja: Ni ujazo wa viganja viwili vya mtu wa kati na kati, wa tende au ngano, kwa kila muislamu; aliye huru na mtumwa, mwanaume na mwanamke, mdogo na mkubwa, na hii ni kwa yule ambaye anachakula kinachozidi kwa siku yake hiyo na usiku wake, kwake yeye na kwa wale anaowahudumia. Na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala ya Iddi.
Mafunzo: Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakat…
- Zakatul-fitiri ya Ramadhani ni lazima kutolewa kwa mtoto na mkubwa, na aliye huru na mamluki, na anasemeshwa hapa msimamizi na bosi, na anaitoa mwanaume kwa niaba yake na watoto wake na wale ambao ni wajibu kwake kuwahudumia.
- Si wajibu zakatul-fitiri kwa kichanga kilichoko tumboni, bali inapendeza tu.
- Kumebainishwa kinachotolewa katika zakatul-fitiri, nakuwa ni chakula cha watu walichokizoea.
- Uwajibu wa kuitoa kabla ya swala ya Iddi, na bora zaidi iwe asubuhi ya siku ya Iddi, na inafaa kuitoa kabla ya Iddi kwa siku moja au mbili.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Zaka.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Zakaatul Fitri.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
أستغفر الله
Je demande pardon à Allah