Atakayesahau hali yakuwa kafunga akala au akanywa, basi atimize swaumu yake, kwani Mwenyez…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Atakayesahau hali yakuwa kafunga akala au akanywa, basi atimize swaumu yake, kwani Mwenyez…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Atakayesahau hali yakuwa kafunga akala au akanywa, basi…
Maelezo ya hadith: Atakayesahau hali yakuwa kafunga akala au akanywa, basi…
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekula au kunywa kwa kusahau akiwa kafunga swaumu ya faradhi au sunna basi atimize swaumu yake wala asifungue; kwa sababu hakukusudia kufungua, bali hiyo ni riziki Mwenyezi Mungu kamsogezea na akamlisha na kumnywesha.
Mafunzo: Atakayesahau hali yakuwa kafunga akala au akanywa, basi…
- Kukubalika kwa swaumu ya aliyekula au kunywa kwa kusahau.
- Hana dhambi aliyesahau akala au kunywa; kwa sababu hilo si kwa maamuzi yake.
- Upole wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake na kuwafanyia wepesi juu yao na kuwaondolea tabu na uzito juu yao.
- Hafungui mfungaji kwa chochote katika vile vyenye kufunguza ila zikikamilika sharti tatu: Ya kwanza: Awe anajua, akiwa mjinga hafungui, ya pili: Awe na kumbukumbu, kama kasahau swaumu yake ni sahihi na wala halazimiki kulipa, ya tatu: Iwe kwa hiari yake, na si kwa kulazimishwa, yaani atumie vyenye kufunguza kwa hiari yake mwenyewe.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Funga.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Vyenye kuharibu Funga.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
اللهم صل على محمد
Ô Allah prie sur Muhammad