Mtakapouona basi fungeni, na mtakapouona basi fungueni, ukifunikwa kwenu nyinyi basi ukadi…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Mtakapouona basi fungeni, na mtakapouona basi fungueni, ukifunikwa kwenu nyinyi basi ukadi…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Mtakapouona basi fungeni, na mtakapouona basi fungueni,…
Maelezo ya hadith: Mtakapouona basi fungeni, na mtakapouona basi fungueni,…
Alibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuingia kwa mwezi wa Ramadhani na kutoka kwake, akasema: Mtakapouona mwandamo wa Ramadhani basi fungeni, yakikukingeni mawingu kati yake na nyie, basi hesabuni siku thelathini za mwezi Shaaban, na mkiuona mwandamo wa mwezi Shawal basi fungueni, yakikukingeni mawingu na ukafichikana kwenu; basi hesabuni siku thelathini za mwezi Ramadhani.
Mafunzo: Mtakapouona basi fungeni, na mtakapouona basi fungueni,…
- Kinachotakiwa ni kutegemea kuona na si hesabu katika kuthibitisha kuingia kwa mwezi.
- Amenukuu bin Mundhiri makubaliano ya wanachuoni kuwa hakuna ulazima wa kufunga ikiwa kuingia kwa mwezi wa Ramadhani ni kwa hesabu pekee pasina kuuona.
- Ulazima wa kukamilisha mwezi Shaaban siku thelathini pindi mawingu au mfano wake yatakapoziba kuuona mwandamo wa mwezi Ramadhani.
- Mwezi unaozingatia mwandamo hauwi isipokuwa ni siku ishirini na tisa, au siku thelathini.
- Ulazima wa kukamilisha Ramadhani siku thelathini mawingu au mfano wake yatakapoziba kati yake na mwandamo wa Shawal.
- Atakayekuwa katika mazingira ambayo hakuna mtu wa kufuatilia maswala ya waislamu katika swaumu, au akawa ni katika watu wanaopoteza kumbukumbu, basi analazimika kulichunga hilo na afuatilie kwa mtu atakayemthibitishia hilo kwa kuuona au kwa mtu mwingine kuuona, atafunga na kufungua kwa taarifa hiyo.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Funga.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Kuuona Mwezi.
بسم الله الرحمن الرحيم
mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
لا حول ولا قوة إلا بالله
Pas de force ni de puissance sauf en Allah