Hakuna Muislamu yeyote atafikiwa na Sala ya lazima kisha akaufanya vizuri udhu wake, na Un…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Hakuna Muislamu yeyote atafikiwa na Sala ya lazima kisha akaufanya vizuri udhu wake, na Un…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Hakuna Muislamu yeyote atafikiwa na Sala ya lazima kish…
Maelezo ya hadith: Hakuna Muislamu yeyote atafikiwa na Sala ya lazima kish…
Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hakuna muislamu atakayekutwa na wakati wa swala ya faradhi akatawadha vizuri udhu wake na ukaukamilisha, kisha akawa na unyenyekevu ndani ya swala yake kiasi kwamba ukawa moyo wake na viungo vyake vyote vimeelekea kwa Mwenyezi Mungu akivuta picha ya utukufu wake, na akatimiza vitendo vya swala kama rukuu na sijida na vinginevyo, isipokuwa swala hii itakuwa ni kifutio cha madhambi madogo madogo yaliyokuwa kabla yake, madam hajafanya dhambi katika madhambi makubwa, na fadhila hii ni endelevu kwa muda wote na katika kila swala.
Mafunzo: Hakuna Muislamu yeyote atafikiwa na Sala ya lazima kish…
- Swala inayofuta madhambi ni ile ambayo mja katawadha vizuri udhu wake, na akaitekeleza kwa unyenyekevu akitafuta radhi za Mwenyezi Mungu kwa swala hiyo.
- Fadhila za kudumu katika ibada, nakuwa ibada ni sababu ya kusamehewa madhambi madogo.
- Fadhila za kutawadha vizuri, na kuswali vizuri pamoja na utulivu ndani yake.
- Umuhimu wa kuyaepuka madhambi makubwa ili kusamehewa madhambi madogo.
- Madhambi makubwa hayafutwi ila kwa toba.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Sala.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Fadhila za Swala.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
حسبنا الله ونعم الوكيل
Allah nous suffit, quel excellent protecteur