Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, atauweka mbali Mwenyezi Mungu uso wa…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, atauweka mbali Mwenyezi Mungu uso wa…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, a…
Maelezo ya hadith: Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, a…
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayefunga siku moja katika Jihadi na kwingineko kwa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa kutafuta thawabu na malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu; basi Mwenyezi Mungu kwa fadhila zake ataweka mbali baina yake na moto miaka sabini.
Mafunzo: Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, a…
- Amesema Nawawi: Fadhila za kufunga katika njia ya Mwenyezi Mungu, na hili linachukuliwa kwa yule ambaye hadhuriki kwa swaumu hiyo, na wala hapotezi haki zake, na wala hatopoteza mapambano yake wala kinginecho katika majukumu mapigano yake.
- Himizo na hamasisho la kufunga swaumu ya hiyari.
- Uwajibu wa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na wala asifunge kwa kujionyesha wala kutaka kusikika, wala kwa makusudio mengine.
- Amesema As-sanadi: Kauli yake "Katika njia ya Mwenyezi Mungu", inategemea kuwa masukudio yake ni nia pekee, na inawezekana kuwa makusudio yake nikuwa amefunga akiwa katika hali ya vitani, na la pili ndio liko karibu na usawa.
- Amesema bin Hajari: Kauli yake: "Viangazi sabini" Kiangazi ni wakati maalumu wa mwaka, na makusudio yake hapa ni mwaka, na kutajwa kiangazi pekee hapa pasina kutaja wakati uliobakia -kama kiangazi na masika, na kipupwe-; kwa sababu kiangazi ndio kipindi kizuri zaidi kwani hua ndio muda wa kuvuna matunda.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Funga.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Funga za Kujikurubisha.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
الله أكبر
Allah est le plus grand