Aliniusia mimi kipenzi changu -rehema na amani ziwe juu yake kwa mambo matatu: kufunga sik…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Aliniusia mimi kipenzi changu -rehema na amani ziwe juu yake kwa mambo matatu: kufunga sik…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Aliniusia mimi kipenzi changu -rehema na amani ziwe juu…
Maelezo ya hadith: Aliniusia mimi kipenzi changu -rehema na amani ziwe juu…
Anaeleza Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa kipenzi chake na jamaa yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuusia na akamsisitizia mambo matatu:
La kwanza: Kufunga siku tatu katika kila mwezi.
La pili: Rakaa mbili za Dhuhaa kila siku.
La tatu: Kusali witiri kabla ya kulala; na hii ni kwa mtu atakayehofia kutoamka mwisho wa usiku.
Mafunzo: Aliniusia mimi kipenzi changu -rehema na amani ziwe juu…
- Kutofautiana kwa usia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Masahaba zake: Hii inasababishwa na elimu yake rehema na amani ziwe juu yake ya kujua hali za Masahaba zake, na kile kinachomfaa kila mmoja miongoni mwao, mwenye nguvu kinachomfaa ni Jihadi, na mchamungu kinachomfaa ni ibada, na mwanachuoni kinachomfaa ni elimu, na kuendelea.
- Amesema bin Hajari Al-Asqalaani: Katika kauli yake: Kufunga siku tatu katika kila mwezi, kinachoonekana nikuwa makusudio yake ni masiku meupe, ambayo ni: Siku ya tarehe kumi na tatu, kumi na nne, na kumi na tano, katika kalenda ya Hijiria.
- Amesema bin Hajari Al-Asqalani: Hapa inaonyesha kuwa inapendeza kuitanguliza witiri kabla ya kulala, na hii kwa mtu ambaye hana uhakika wa kuamka kuswali.
- Umuhimu wa matendo haya matatu; kwa sababu ya usia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwausia idadi kubwa ya Maswahaba zake.
- Amesema bin Daqiq Al-Iid katika kauli yake: "Na rakaa mbili za Dhuha": Huenda kataja chache ambazo unapatikana msisitizo wa kuzifanya, na katika hili kuna dalili ya kuwa Dhuha ni sunna, nakuwa kwa uchache ni rakaa mbili.
- Wakati wa swala ya Dhuha: Ni baada ya kuchomoza Jua kwa robo saa takriban, na unakwenda wakati wake mpaka kabla ya Adhuhuri kwa dakika kumi takriban, na idadi: Kwa uchache ni rakaa mbili, na zimetofautiana kauli za wanachuoni kuhusu wingi wake; wakasema: Rakaa nane, na wakasema: Hakuna kiwango cha wingi wake.
- Wakati wa witiri: Baada ya swala ya Ishaa mpaka kuchomoza Alfajiri, na uchache wake ni rakaa moja, na wingi wake ni rakaa kumi na moja.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Funga.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Funga za Kujikurubisha.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
أستغفر الله
Je demande pardon à Allah